Skip to main content
Skip to main content

Njuki aahidi kulinda ugatuzi na kutetea maslahi ya kaunti

  • | Citizen TV
    441 views
    Duration: 1:20
    Gavana wa Tharaka Nithi Muthomi Njuki ndiye mwenyekiti mpya wa Baraza la Magavana nchini. Njuki ameahidi kulinda ugatuzi, kuimarisha uchumi na kutetea maslahi ya kaunti. Akizungumza baada ya kukabidhiwa uongozi na Gavana wa Wajir Ahmed Abdullahi, Njuki ameahidi kushirikiana na mabunge yote mawili kutatua mizozano kuhusu mgao wa fedha, kuchelewa kwa fedha za kaunti na ugavi wa rasilimali za kitaifa. Pia ameahidi kushinikiza ongezeko la mgao wa fedha kwa kaunti kutoka shilingi bilioni 400 za sasa hadi shilingi bilioni 500 katika mwaka ujao wa kifedha.