Skip to main content
Skip to main content

ODM yataka nafasi ya naibu rais 2027

  • | Citizen TV
    6,237 views
    Duration: 3:20
    Viongozi wa chama cha ODM wamesisitiza kuwa nafasi ya naibu rais katika Uchaguzi Mkuu ujao ni ya chama hicho. Naibu kinara wa ODM, Simba Arati, na kiongozi wa wachache katika Bunge la Kitaifa, Junet Mohamed, wanasema chama hicho kinataka kupewa nafasi ya naibu rais pamoja na nusu ya nafasi za mawaziri, makatibu wakuu na mabalozi kama sehemu ya ushirikiano wake wa kisiasa. Viongozi hao wanasema hatua hiyo itakiwezesha ODM kumpigia debe Rais William Ruto katika azma yake ya kutetea urais na kuchaguliwa tena. Mwanahabari wetu wa masuala ya kisiasa, Stephen Letoo, ana taarifa hiyo.