Askofu Mkuu wa Kanisa la Kianglikana nchini, Jackson Ole Sapit, ameitaka idara ya usalama kudhibiti taifa mikononi mwa wahuni wanaozidi kuvuruga mikutano ya kisiasa.
Akizungumza katika Kaunti ya Kisii, Ole Sapit amesema uhasama wa kisiasa unaozidi kushuhudiwa nchini unatia wasiwasi na unapaswa kukomeshwa mara moja.
Ameonya kuhusu hofu ya machafuko ya kisiasa mwaka mmoja kabla ya uchaguzi mkuu. Alikuwa akizungumza katika hafla ya ufunguzi rasmi wa kongamano la kila mwaka la vijana wa Kanisa la Kianglikana nchini.