Skip to main content
Skip to main content

Polisi wakana madai ya kulinda wahuni kwenye mikutano ya upinzani

  • | Citizen TV
    4,947 views
    Duration: 3:20
    Idara ya polisi sasa inakana madai kuwa imefumbia macho visa vya uhuni na vurugu za vijana kwenye mikutano ya viongozi wa upinzani. Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi Eliud Lagat amekana madai kuwa polisi wanatumiwa kuvuruga mikutano ya wapinzani na kulinda magenge ya wahuni. Akizungumza alipokuwa akikagua maandalizi ya mahafali katika shule ya mafunzo ya polisi ya Kiganjo huko Nyeri, Lagat amesema idara hiyo imeweka mikakati ya kuwakabili wahuni na kuhakikisha kuwa uchaguzi mkuu na taifa liko salama.