Skip to main content
Skip to main content

Pwani yapigania nafasi ya naibu rais 2027

  • | Citizen TV
    1,035 views
    Duration: 2:43
    Viongozi kutoka eneo la Pwani wamezidisha juhudi za kutaka eneo hilo lipate nafasi ya naibu rais katika Uchaguzi Mkuu ujao. Katika mikutano iliyofanyika kaunti za Lamu na Tana River, viongozi hao walihimiza wakazi wa Pwani kujisajili kwa wingi kama wapiga kura ili kuimarisha ushawishi wa eneo hilo kisiasa. Aidha, wamemtaja Waziri wa Madini, Ali Hassan Joho, kama mgombea anayefaa kushika nafasi hiyo. Wakizungumza mjini Lamu, viongozi hao pia walitetea mradi wa kiwanda cha kusafisha mafuta, wakisema unatarajiwa kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kuongeza nafasi za ajira kwa wakazi wa eneo hilo. Francis Mtalaki ana taarifa hiyo.