- 2,813 viewsDuration: 1:52Rais william ruto amewataka wapinzani wake kueleza mpango na ajenda yao kwa wakenya, akisisitiza kwamba hawana maono yoyote kwa taifa. Rais ruto ambaye yuko kwenye ziara ya siku 10 katika ngome yake ya eneo la kaskazini mwa bonde la ufa, amesema yuko tayari kwa uchaguzi mkuu wa mwaka ujao akisisitiza kwamba ametekeleza manifesto yake aliyoahidi mwaka wa 2022. Ruto ameanza ziara yake katika kaunti ya nandi na baadaye anatarajiwa kule uasin gishu.