- 29,239 viewsDuration: 3:10Mwakilishi wa kike kaunti ya Kisumu Ruth Odinga amemtetea katibu mkuu wa chama cha ODM Edwin Sifuna akisema anapigwa vita na watu wanaotaka kukinadi chama cha ODM kwa rais william ruto. Kupitia kwa ujumbe mtandaoni, Ruth Odinga ambaye ni dadake aliyekuwa waziri mkuu hayati Raila Odinga, alidai serikali imekuwa ikifadhili mikutano ya ODM ili kuwashawishi wafuasi wake kumuunga mkono rais ruto katika uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.