- 2,576 viewsDuration: 2:32Rais William Ruto amekashifu upinzani kwa kupinga miradi ya maendeleo ya serikali, akisema baadhi ya wanasiasa wanatumwa kupinga kila juhudi za serikali. Akizungumza katika kaunti ya Taita Taveta, Ruto amesema wapinzani wake hawana ufahamu wa kutosha kuhusu miradi hiyo na amewataka kuwasilisha sera mbadala badala ya kuendeleza siasa za chuki na kuigawanya nchi kwa misingi ya kikabila. Francis Mtalaki ana taarifa zaidi.