- 2,994 viewsDuration: 2:33Rais William Ruto amewaonya wanasiasa dhidi ya kuwahusisha polisi na asasi za usalama katika siasa, akisema idara hizo zinafaa kulinda demokrasia na haki za wananchi kuelekea uchaguzi mkuu wa 2027. Akizungumza alipokuwa akiongoza sherehe ya 50 ya kufuzu kwa makurutu wa GSU katika Chuo cha Kitaifa cha Polisi, Embakasi, Nairobi, Rais Ruto aliwataka maafisa hao kutekeleza majukumu yao kwa kutopendelea upande wowote na kuheshimu haki za kikatiba za wananchi.