- 2,125 viewsDuration: 2:26Mdhibiti wa bajeti margaret nyakang’o ameibua maswali kuhusu matumizi yasiyofaa ya serikali kwenye safari za humu nchini na nje ya nchi. Nyakang'o anasema serikali ilitumia shilingi bilioni 25 kwenye safari hizo. Haya yanajiri mwaka mmoja tu baada ya rais ruto kutangaza kwamba serikali itapunguza gharama hiyo kwa asilimia 50. Emmanuel too anatufungulia jamvi la nipashe kwa taarifa hiyo.