- 777 viewsDuration: 1:17Serikali itawalipia wakenya milioni 1.5 matozo ya bima ya afya - sha kuanzia wiki ijayo. Haya ni kwa mujibu wa rais william ruto ambaye amesema kuwa watakaofaidika na mpango huo ni wale ambao hawana uwezo wa kulipia sha. Aidha rais ruto amesema atafanya mkutano na magavana na wabunge ili wao pia wawalipie pesa hizo wakenya wengine milioni moja. Aliongeza kwamba hatua hiyo inalenga kuwawezesha wakenya wote kupata matibabu bila malipo.