- 860 viewsDuration: 2:54Serikali imeondoa hofu kuwa ugonjwa wa Ebola umefika nchini. Waziri wa Afya Aden Duale amesema hakuna visa vilivyothibitishwa nchini kwa sasa. Duale amewataka Wakenya kuepuka safari zisizo za lazima katika mataifa yaliyoathiriwa na mlipuko huo, ikiwemo Democratic Republic of the Congo. Aidha, amesema serikali imeweka tahadhari maalum katika kaunti 22 zinazotajwa kuwa katika hatari kubwa ya kukumbwa na maambukizi ya ugonjwa huo.