- 5,603 viewsDuration: 3:36Hatua ya shirika la kusambaza maji Pwani -Coast Water- kusitisha huduma zake katika kaunti za Taita Taveta, Kilifi na Kwale, imezua hisia kali kutoka kwa wakazi pamoja na serikali za kaunti hizo. Uamuzi huo wakosolewa huku uongozi wa kaunti hizo ukisema kuwa ni ukiukaji mkubwa wa sheria. Wakazi wanahofia kuwa wataendelea kutaabikia maji hata zaidi, ikizingatiwa kuwa wakazi haswa katika maeneo ya Voi na viunga vyake tayari wanalazimika kununua maji