- 262 viewsDuration: 1:05Ukosefu wa maji safi na vifaa bora vya usafi wa mazingira unaendelea kuwa tishio kubwa kwa afya na elimu ya watoto katika shule za msingi za mashinani kaunti ya vihiga. Katika shule ya msingi ya Mwituha, wanafunzi hulazimika kubeba maji kutoka nyumbani kila siku huku shule hiyo ikipungukiwa pia na vyoo. Wazazi, walimu pamoja na maafisa wa afya sasa wanaonya kuhusu hatari ya kuongezeka kwa magonjwa yanayotokana na maji machafu.