- 14,505 viewsDuration: 2:36Seneta wa Kaunti ya Nairobi Edwin Sifuna amemtaka Gavana Johnson Sakaja kufutilia mbali mkataba aliotia sahihi jana na serikali kuu kuhusu ushirikiano wa utendakazi wa kaunti. Sifuna ameutaja ushirikiano huo kuwa kinyume na sheria na kwamba ataongoza pingamizi dhidi ya ushirikiano huo hadi mahakamani. Kwenye ushirikiano huo Rais William Ruto amependekeza kubuniwa kwa kamati inayohusisha mawaziri watakaosaidia katika utendakazi wa kaunti pamoja na kuahidi kutoa shilingi bilioni 80 zaidi kwa maendeleo. Mbunge wa Embakasi East Babu Owino pia anashikilia kauli ya Sifuna kuwa mkataba wa ushirikiano unakiuka sheria na muongozo wa kaunti.