- 16,703 viewsDuration: 41sTazama namna simba huyu alivyookolewa baada ya kuangukia kwenye kisima cha mita 9 katika jimbo la magharibi la Gujarat, India. Maafisa wa idara ya misitu walifika haraka katika wilaya ya Somnath baada ya wakazi wa eneo hilo kumwona mnyama huyo ambaye alikuwa ameangukia kwenye kisima kilicho wazi wakati wa usiku. Simba huyo aliyeokolewa baadaye alipelekwa katika kituo cha karibu cha huduma kwa wanyamapori kisha aliachiliwa tena kurudi porini. #bbcswahili #indiasimba #wanyama Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw