Skip to main content
Skip to main content

Tafakari Ya Babu: Tajiri na maskini

  • | Citizen TV
    4,343 views
    Duration: 2:06
    Yatafakari haya... Anasema babu yangu: Mtu maskini, au mchochole, kila siku huamka mapema. Husema anakwenda kutafuta unga au kuchimba riziki. Tajiri humtumia vibaya huyu maskini; tajiri ana mali zake, maskini ana nguvu zake. Tajiri hufanyiwa kazi na kumlipa mchochole ujira wa mkia wa mbuzi—hauwafukuzi nzi wala kuziba makalio. Mwanajeshi na polisi huwalinda wote wawili, maskini na tajiri. Mlipa ushuru huwalipia wote watatu. Benki nazo huwanufaikia wote kwa hiari yao. Husema, "Weka pesa zako zote kwetu; zitakuwa salama na pia zitazaa faida. Ukihitaji, tutakukopesha." Wakili naye huwashawishi wote kwa maneno ya hila. Atakuambia, "Ulikwenda kujisaidia msituni ukidhani unaweka mbolea, lakini sheria inasema umeharibu mazingira. Utatiwa hatiani, lakini mimi nitakutetea." Daktari naye huwatisha kwa afya zao. Atasema, "Huna damu ya kutosha mwilini. Umefikaje hadi hapa? Unahitaji kulazwa hospitalini, na pia utahitaji oksijeni." Mwishowe, wanakuuzia hewa ambayo Mwenyezi Mungu aliiumba bure. Mwizi naye huwatishia wote kwa kuwaibia walichonacho, hata yule mchochole. Lakini mwanasiasa huja juu ya jasho la wote hao. Hujipa jina na hadhi kubwa, akijiita "Mheshimiwa", kisha huwahonga ili wamchague na kupata cheo. Yatafakari hayo.