- 4,770 viewsDuration: 3:20Uamuzi wa Mahakama kuhusu kutimuliwa kwa aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua umeibua mgogoro wa kisheria na kikatiba. Mawakili wamekosoa uamuzi huo wa majaji watatu, waliobaini kuwa haki za kimsingi za Gachagua zilikiukwa kwenye mchakato wa kumwondoa afisini, ila wakakataa kutupilia mbali uamuzi wa Senate of Kenya. Wakosoaji wanasema kuwa japokuwa majaji hao walitaka kuzuia msukosuko wa kisiasa, waliibua mtafaruku wa kikatiba.