- 4,173 viewsDuration: 2:53Siku moja tu baada ya mwanamke mmoja kufariki na wengine wawili kukwama ndani ya mgodi wa dhahabu wa Lomeguro, Turkana Kaskazini, mpasuko mkubwa wa ardhi umetokea eneo hilo na kusababisha machimbo mengi kuporomoka. Kamishna wa kaunti ya Turkana, Julius Kavita, amezuru eneo hilo na kuamuru shughuli zote za uchimbaji wa dhahabu kusitishwa mara moja. Cheboit Emmanuel ana maelezo zaidi kutoka Turkana.