Skip to main content
Skip to main content

Uhaba wa mafuta wazikumba nchi kadhaa huku Kenya ikitaja athari za vita vya Ghuba

  • | Citizen TV
    4,539 views
    Duration: 3:32
    Mataifa kadhaa yanashuhudia uhaba wa mafuta, hali inayolemaza shughuli za usafiri huku wamiliki wa magari nchini Ethiopia, Burundi na Mozambique wakilazimika kusitisha baadhi ya huduma za usafiri wa umma. Hapa nchini, Waziri wa Hazina Kuu ya Kitaifa John Mbadi, akizungumza Kaunti ya Siaya, amesema vita vya Ghuba vimekatiza asilimia 20 ya usambazaji wa mafuta duniani. Mbadi amesema Kenya sasa inategemea kampuni tatu za usambazaji wa mafuta kutoka nje ili kuhakikisha upatikanaji wa mafuta nchini.