- 1,719 viewsDuration: 3:03Uhaba wa maziwa unaoshuhudiwa nchini huenda ukaendelea kwa zaidi ya mwezi mmoja, huku baadhi ya maduka yakisalia bila bidhaa hiyo muhimu. Kulingana na Bodi ya Maziwa, kiwango cha maziwa kinachowasilishwa kwa kampuni za maziwa kimepungua kwa takriban lita milioni tisa katika kipindi cha miezi miwili iliyopita. Ukosefu wa mvua na wakulima kuuza maziwa moja kwa moja kwa wateja badala ya kupitia kampuni umechangiwa na upungufu huo.