- 2,350 viewsDuration: 3:08Wanasiasa wa upinzani sasa wanadai kuwa visa vya wahuni kutibua mikutano ni njama ya serikali ya Kenya Kwanza kuchelewesha uchaguzi ujao na kuongeza muda wake wa uongozi. Kinara wa DCP Rigathi Gachagua na Gavana wa Siaya James Orengo wanadai mpango huo unahusisha Tume ya Uchaguzi na asasi za usalama, ambazo wanasema zimeshindwa kuwachukulia hatua wahuni. Wanasiasa hao wa upinzani pia wameendelea kukosoa vurugu zilizoshuhudiwa wikendi katika Kaunti ya Homa Bay.