Skip to main content
Skip to main content

Upinzani wakosoa utekelezaji wa Katiba miaka 16 baadaye

  • | Citizen TV
    1,737 views
    Duration: 3:08
    Hata hivyo, kwa viongozi wa upinzani na wanaharakati wa kutetea haki, hakukuwa na mengi ya kusherehekea siku hii ya kuangazia hatua zilizopigwa katika utekelezaji wa Katiba ya sasa. Majaji wakuu wastaafu David Maraga na Willy Mutunga ni miongoni mwa wanaozidi kulalamikia ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu, miaka 16 baada ya Katiba mpya kuanza kutekelezwa. Kinara wa Wiper, Kalonzo Musyoka, ameikosoa serikali kwa kushindwa kufanikisha kikamilifu ugatuzi, ambao ulikuwa nguzo muhimu ya Katiba hiyo.