- 7,294 viewsDuration: 2:53Viongozi wa upinzani wamemkosoa Rais William Ruto wakidai kuwa ndiye mfaidi mkuu wa mkataba wa mafuta wa serikali kwa serikali (G-to-G). Wakiongozwa na kinara wa DAP-K Eugene Wamalwa na mwenzake wa Peoples Party of Kenya, Ndindi Nyoro, katika hafla tofauti, viongozi hao wameendelea kuilaumu serikali huku wakimpongeza Rais wa Uganda Yoweri Museveni kwa kufichua kile walichodai kuwa ni kuwepo kwa wasuluhishi katika mpango huo.