- 770 viewsDuration: 1:51Usahihisaji wa shule kwa wale watakaojiunga na gredi ya kumi utaanza Jumanne wiki hii. Katibu katika wizara ya Elimu Profesa Julius Bitok amesema kuwa uteuzi wa wanafunzi kujiunga na gredi ya kumi ulifanywa kwa mashine na sababu mbalimbali huenda zimesababisha kutoridhika kwao na shule walizopata. Aidha Bitok amekiri kuwa kuna baadhi ya wanafunzi ambao wameteuliwa katika shule za jinsia zisisofaa na kuwataka wadau kuwa na subra huku usahihishaji ukiendelea.