- 309 viewsDuration: 2:47Idadi ya watoto wanaojiunga na shule za chekechea imeongezeka katika Kiambu County katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, kufuatia uwekezaji mkubwa katika sekta ya elimu ya awali. Kulingana na Gavana Kimani Wamatangi, ujenzi wa madarasa mapya, kuboreshwa kwa miundombinu na utoaji wa lishe bora umechangia kuimarika kwa elimu ya watoto wadogo na kuongeza idadi ya wanaoandikishwa katika shule za chekechea.