- 3,594 viewsDuration: 7:18Kwa miezi miwili sasa, familia saba katika kaunti za Kiambu na Nyandarua zimeachwa na majonzi baada ya wapendwa wao kufariki kwa kubugia pombe haramu. Eneo la Kimende liliathirika zaidi mwezi uliopita baada ya watu wanne pia kufariki baada ya kubugia pombe haramu katika eneo hilo. Ni matukio ambayo yameibua maswali kuhusu kurejea kwa pombe haramu nchini huku takwimu kutoka Halmashauri ya Kupambana na Mihadarati (NACADA) zikionyesha idadi ya pombe haramu iliyonaswa imeongezeka katika muda wa miaka minne iliyopita. Mwanahabari wetu Gatete Njoroge alivalia njuga taswira hii kubaini hali ilivyo.