- 7,735 viewsDuration: 1:52Shinikizo za kuondolewa kwa kiongozi wa wachache katika bunge la taifa Junet Mohammed zinashamiri huku tetesi za malumbano katika chama cha ODM na muungano wa Azimio La Umoja One Kenya zikisheheni. Hii leo, vyama saba vya muungano huo vinataka shughuli hiyo ya kuondolewa kwa Junet iharakishwe na nafasi hiyo kuchukuliwa na baadhi ya wabunge wa upinzani. Aidha, wanadai, Junet hashughulikii maswala ya upinzani ila anajipendekeza kwa rais Kadhalika, wanamtaka kiongozi wa Azimio rais mstaafu Uhuru Kenyatta kuita mkutano wa vyama tanzu kwa mipango ya uchaguzi ujao wa 2027