- 2,814 viewsDuration: 3:27Visa vya vifo vya mahabusu waliokuwa wakizuiliwa katika seli za polisi vimezua wasiwasi nchini, huku mamlaka ya IPOA ikianzisha uchunguzi kuhusu matukio matatu tofauti yaliyotokea katika vituo vya polisi vya Kibera, Kariobangi North na Kiambu. Uchunguzi wa maiti ya Brian Njunge, aliyekuwa akizuiliwa katika kituo cha Kiambu kabla ya kifo chake, umebaini kuwa alifariki kutokana na kunyongwa. Wakati huo huo, uchunguzi wa maiti ya Peter Kiiru aliyefariki katika kituo cha polisi cha Kariobangi North na Bernard Nyakwama Omae aliyefariki katika kituo cha Kibera unatarajiwa kufanyika baadaye wiki hii.