- 158 viewsDuration: 1:48Ili kuhakikisha vita dhidi ya dawa za kulevya, pombe haramu zimefaulu, wanasiasa katika kaunti ya Nyeri wametahadharishwa dhidi ya kuviingilia vita hivi, kwa kuwalinda wafanyabiashara ambao tayari wamelengwa. Akiwatolea onyo wanaoendeleza biashara hii alipofanya kikao na kamati ya usalama , kamishna wa kaunti ya Nyeri Joseph Biwott, ametaja ufisadi kama kizingiti kikubwa dhidi ya vita hivi, akiapa kuwapiga kalamu maafisa watakaopatikana kula rushwa eneo hilo.