- 1,582 viewsDuration: 3:13Mkutano wa wajumbe wa chama cha madaktari Kenya Medical Practitioners, Pharmacists and Dentists Union (KMPDU) ulikumbwa na vurugu baada ya kundi moja la madaktari kupinga kuapishwa kwa viongozi wapya waliochaguliwa hivi maajuzi. Madaktari hao walilalamika kuwa sheria za chama hazikufuatwa katika shughuli hiyo na kupinga kuapishwa kwa viongozi hao. Hata hivyo, madai hayo yamepuuzwa na viongozi wa chama hicho wakisema wanaolalamika hawakualikwa kuhudhuria mkutano huo.