Skip to main content
Skip to main content

Waathiriwa wa maandamano waipa serikali siku saba kutoa fidia walizoahidiwa

  • | Citizen TV
    1,344 views
    Duration: 1:18
    Jamaa na waathiriwa wa maandamano wameipa serikali siku saba kutoa fidia walizoahidiwa, la sivyo waandamane kuanzia tarehe 16 hadi 25 Juni. Kupitia mawakili wao, waathiriwa hao wamemkosoa Rais William Ruto kwa kile walichokitaja kuwa ahadi zisizotekelezwa, licha ya kuahidi hadharani kuwa waathiriwa wote wa maandamano watafidiwa kufikia mwezi huu. Misimamo hii ikijiri takriban wiki moja baada ya Tume ya Kitaifa ya Haki za Binadamu nchini kutangaza kuwa Hazina ya kitaifa bado haijatoa shilingi bilioni mbili zilizotengwa kwa fidia zao