- 994 viewsDuration: 1:48Waathiriwa na manusura wa ukatili wa polisi wamepuuzilia mbali kauli ya Rais William Ruto ya kujutia dhulma dhidi yao, wakitaka hatua madhubuti zichukuliwe dhidi ya wahusika katika mauaji na kutoweka kwa Wakenya. Wakizungumza jijini Nairobi, waathiriwa hao wametaka uchunguzi huru, fidia kamili na mashtaka dhidi ya polisi waliohusika. Wanasema zaidi ya visa 536 vya mauaji ya kiholela na visa 111 vya kutoweka kwa lazima, vimerekodiwa.