- 398 viewsDuration: 1:15Huku shamrashamra za krismasi zikiendelea, wafanyabiasahara na wachuuzi kaunti ya Mombasa wanalalamikia kuhangaishwa na maafisa wa kaunti wanaowafurusha kutoka maeneo wanayotegemea kupata riziki zao. Wafanyabiashara hao wametoa wito kwa serikali ya kaunti kutoa mwelekeo wa sehemu mwafaka za kufanyia biashara. Kadhalika, wamelalamikia ukosefu wa maji safi kaunti ya Mombasa.