Skip to main content
Skip to main content

Wafanyabiashara wa Nairobi waandamana kupinga ongezeko la ushuru

  • | Citizen TV
    13,721 views
    Duration: 3:26
    Shughuli za biashara katikati ya jiji la Nairobi zilisitishwa kwa saa kadhaa huku wafanyibiashara wakiandamana kulalamikia ongezeko la ushuru kwa bidhaa zinazoagizwa kutoka nje. Wafanyibiashara hao walifunga biashara zao na kuingia mitaani, japo polisi walitibua azma yao ya kufika katika makao makuu ya kukusanya ushuru -KRA- kuwasilisha malalamishi yao. Wafanyibiashara hao walirushiwa vitoa machozi na kulazimika kutawanyika huku mamlaka ya KRA iikitetea kodi hiyo.