- 9,233 viewsDuration: 3:45Eneo bunge la Ol Kalou limeshuhudia kampeni za aina yake katika siku za hivi karibuni huku wanaogombea kiti cha ubunge wakimwaga fedha baada ya mikutano ya kampeni. Wakazi wamevuna pakubwa kutokana na hali hiyo, huku miradi mbalimbali ya serikali ikionekana kuharakishwa ili kuwafikia wananchi. Na kama anavyotujengea taswira Emmanuel Too, minofu ya kampeni inaendelea kutafunwa huku Mbunge wa Nakuru Town East, David Gikaria, akikiri hadharani kuwa alitumia zaidi ya shilingi milioni moja katika hafla moja ya kisiasa iliyofanyika katika eneo hilo.