- 338 viewsDuration: 2:31Hafla maalum ya kuwaenzi na kuwatambua wanahabari na watangazaji wakongwe inatarajiwa kuandaliwa nchini mwezi Septemba mwaka huu. Katika uzinduzi wa hafla hiyo, mtangazaji Fred Obachi Machoka, anayeadhimisha miaka 50 katika tasnia ya utangazaji, amesema ni muhimu kuwakumbuka na kuwatambua wale waliojitolea kulitumikia taifa kupitia taaluma hiyo. Baraza la Habari Kenya, MCK, linashirikiana na Machoka katika maandalizi ya hafla hiyo. Powel Okunyo anaripoti.