Skip to main content
Skip to main content

Washukiwa wa uvamizi wa kanisa Kisumu waachiliwa

  • | Citizen TV
    1,061 views
    Duration: 1:51
    Watu wanane waliokuwa wamekamatwa kuhusiana na jaribio la kuvamia Kanisa la St. Stephen's jijini Kisumu wameachiliwa huru baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuwafungulia mashtaka. Akitoa uamuzi huo, Hakimu Mkuu Mwandamizi Valerie Adhiambo alitupilia mbali maombi matatu ya dharura yaliyowasilishwa mahakamani, yakiwemo ya upande wa mashtaka ya kuendelea kuwazuilia washukiwa hao wakisubiri hatua zaidi za kisheria. Mawakili wa washukiwa walipongeza uamuzi huo na kutoa wito kwa polisi kuwakamata waliohusika kupanga na kutekeleza shambulizi hilo. Watu wawili walifariki dunia baada ya makundi mawili ya vijana kukabiliana nje ya Kanisa la St. Stephen's tarehe 12 Julai, wakati viongozi wa upinzani walipokuwa wakihudhuria hafla ya kuchangisha fedha kanisani.