Washukiwa wanane wanaodaiwa kuhusika na uuzaji wa mbolea iliyoharibika wanazuiliwa na polisi katika Kaunti ya Uasin Gishu baada ya kukamatwa usiku wa Jumamosi.
Akithibitisha kukamatwa kwao, Kamishna wa Kaunti ya Uasin Gishu, Edison Yale, alisema magunia 4,000 ya mbolea iliyoharibika yalipatikana wakati wa operesheni maalum iliyofanywa katika maeneo mbalimbali ya kaunti hiyo.
Mamlaka zimewataka wakulima kuwa waangalifu wanaponunua mbolea na kuhakikisha wanainunua kutoka kwa wauzaji walioidhinishwa pekee ili kuepuka hasara.
Laura Otieno ana taarifa zaidi.