Skip to main content
Skip to main content

Watu wanne waaga dunia katika ajali ya Karatina–Nanyuki

  • | Citizen TV
    2,308 views
    Duration: 1:35
    Watu wanne wameaga dunia na wengine saba kujeruhiwa kufuatia ajali ya barabarani katika eneo bunge la Kieni, kwenye barabara kuu ya Karatina–Nanyuki usiku wa kuamkia leo. Ajali hiyo inaripotiwa kutokea baada ya basi la kampuni ya Mabruk Classics kubingirika mara kadhaa. Waliopoteza maisha, wakiwemo mtoto wa miaka minne na wanaume watatu, walifariki papo hapo. OCPD wa Kieni Mashariki, Maina Kabuthia, amesema basi hilo lilikuwa linasafiri kutoka Nairobi kuelekea Moyale wakati ajali ilipotokea. Kwa upande wake, kampuni ya Mabruk Classics imesema ripoti za awali zinaonyesha kuwa ajali hiyo ilisababishwa na kupasuka kwa gurudumu la basi.