- 10,023 viewsDuration: 2:40Watu wanne wamefariki baada ya lori la kusafirisha mafuta ya petroli kulipuka katika eneo la Turbo, kaunti ya Uasin Gishu. Wawili kati ya waliofariki walipoteza maisha papo hapo walipokuwa wakiteka mafuta kutoka kwa lori hilo lililoanguka jana usiku. Watu wengine 23 walijeruhiwa na wanaendelea kupokea matibabu katika hospitali ya rufaa ya Moi, Eldoret. Boniface Barasa alifuatilia taarifa hii na anatufungulia jamvi la Nipashe jioni ya leo.