Wakenya wamejitokeza kwa wingi makanisani kwa ibada ya krismasi. katika Kanisa la Holy Family, Nairobi, waumini wamesherehekea Sikukuu ya Krismasi, ambapo Padre Robert Chris Ndungu amewahimiza kuzingatia maadili na huruma katika kukumbuka kuzaliwa kwa Yesu Kristo.
Akitoa ujumbe wa msimu wa sikukuu kwa Wakenya wote, Askofu Mkuu Philip Nyolo pia amewataka viongozi, wakiwemo wanasiasa, kuendeleza injili ya amani na kufanya kazi kwa ajili ya ustawi wa taifa na wala si kwa ajili ya matumbo yao binafsi.