Kufikia Sasa asilimia 95 ya vijana humu nchini walio kwenye mpango wa Nyota wameweza kuanzisha biashara maeneo mbalimbali nchini.
Akizungumza wakati wa ziara yake kaunti ya Kirinyaga alipokutana na baadhi ya vijana walioko kwenye mpango huu Waziri Wicliffe Oparanya ameeleza kuwa serikali inampango wa kutoa fedha Zaidi kama mtaji wa kuanzisha biashara kwa vijana. Oparanya ameeleza Awamu ya pili itahusisha kutolewa kwa Shilingi 25,000 nyingine kwa kila aliyenufaika, na hivyo kufanya jumla ya msaada wa kuanzisha biashara kufikia Shilingi 50,000 kwa kila kijana. Afisa mkuu wa mpango huo wa Nyota Henry Rithaa ameelezea kuwa mradi wa NYOTA unafadhiliwa na serikali kupitia benki ya dunia ili kunufaisha vijana kuanzisha biashara na mpango huo unatarajiwa kuendelea hadi mwaka wa 2028.