- 9,931 viewsDuration: 3:22Hali ya taharuki inaendelea kutanda katika eneo la Mwingi, kaunti ya Kitui huku usalama ukizidi kudorora na kusababisha usafiri kwenye barabara ya Mwingi - Garissa kutatizika. Mzozo kati ya jamii mbili jirani ulisababisha kuuawa kwa watu wanane mwishoni mwa wiki. Ghadhabu ya wakazi wa eneo hilo imesababisha kufungwa kwa barabara hiyo huku wasafiri wakisalia kwenye njia panda kwenye ofisi za kampuni za uchukuzi.