- 599 viewsDuration: 3:20familia zaidi ya 2,500 za jamii ya Sengwer zinazoishi katika msitu wa Embobut, Marakwet Mashariki, zinahofia kufurushwa tena baada ya shirika la Huduma kwa Misitu kutoa ilani ya kuwataka waondoke ndani ya wiki moja. Na Kama anavyoarifu Collins Shitiabayi, Jamii hiyo imeitaka serikali kuheshimu uamuzi wa Mahakama ya Rufaa wa mwaka 2021 uliositisha kufurushwa kwa Wasengwer waliokuwa wakiishi msituni humo hadi kesi yao isikizwe na kuamuliwa .