Utunzaji mazingira: Kamati 4 za mawaziri kubuniwa

  • | KBC Video
    6 views

    Kikao cha ngazi za juu cha pande husika kwenye mkutano wa kimataifa kuhusu kuhusu mabadiliko ya tabia nchi kiliashiria kubuniwa kwa kamati nne za mawaziri kujadili masuala manne tata ambayo huenda yakasambaratisha mashauriano baina ya pande hizo. Kamati hizo nne zitaongozwa kwa pamoja na mawaziri wa masuala ya hali ya anga kutoka mataifa yanayostawi na yale yaliyostawi. Kundi la wawakilishi wa Afrika limesema makundi hayo manne yatatafuta mbinu za kutekeleza masuala mbali mbali, masoko ya hewa ya kabon na hatua za pamoja zinazopasa kuchukuliwa. Hayo yalijiri huku muungano wa haki kuhusu mabadiliko ya anga barani Afrika ukitoa wito wa kushirikishwa kwa suala la afya katika malengo tekelezi ya kila taifa.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive