- 611 viewsDuration: 6:03Amekuwa mstari wa mbele kuangazia safari za wanawake wanaofanya shughuli mbalimbali zinazokuza na kuinua jamii hapa runinga ya Citizen. Kupitia kipindi chake cha Mwanamke Bomba, amekuwa akitembea safari hii na wanawake kutoka sehemu mbalimbali ambao amekuwa akiwavisha taji kila wiki. Tunamzungumzia mtangazaji mwenza Mwanahamisi Hamadi ambaye leo twamvisha yeye taji kwa kutajwa kuwa shujaa kwenye sherehe za hapo jana za Mashujaa.