- 58,438 viewsDuration: 1:50Wakati huo huo Gavana wa Nyeri Mutai Kahiga ameomba radhi kwa matamshi yake hapo jana kuhusu kifo cha Raila Odinga. Kahiga ameiomba familia ya Odinga msamaha akisema matamshi yake hayakuwa ya kukejeli kifo chake. Kahiga amesema atabeba msalaba wake na pia ameamua kujiuzulu mara moja kama naibu mwenyekiti wa baraza la magavana. Kahiga amesema anajutia matamshi yake lakini matamshi hayo ya jana ni yake binafsi na wala sio matamshi yanayowakilisha jamii ya mlima kenya.