Skip to main content
Skip to main content

Gavana wa kaunti ya Nyeri Mutahi Kahiga ajiuzulu kama Naibu Mwenyekiti wa baraza la magavana

  • | Citizen TV
    3,110 views
    Duration: 1:37
    Gavana wa kaunti ya Nyeri Mutahi Kahiga leo amejiuzulu wadhifa wake wa Naibu Mwenyekiti wa baraza la magavana. Hatua hiyo inafuatia matamshi yake ya kukejeli kifo cha aliyekuwa waziri mkuu Raila Odinga na ambayo yamevutia hisia kali kutoka kwa Wakenya. Na huku akijutia matamshi yake, Kahiga pia ameiomba familia ya Odinga msamaha akisema matamshi yake hayakuwa ya kukejeli kifo chake. Kahiga amesema atabeba msalaba wake na kwamba matamshi yake ya hapo jana yalikuwa yake binafsi na wala sio matamshi yanayowakilisha jamii ya mlima Kenya.