Watu watatu walifariki kwenye ajali ya ndege Malindi

  • | Citizen TV
    8,242 views

    Watu watatu wamefariki kwenye ajali ya ndege ndogo katika kijiji cha Kwachocha huko Malindi, Kaunti ya Kilifi. Ndege hiyo, ambayo ilikuwa kwenye mafunzo ilipata hitilafu za mitambo na kulazimika kutua kwenye barabara kuu ya Malindi kuelekea Mombasa. Mwendeshaji bodaboda na abiria wake ni miongoni mwa watu waliofariki baada ya kugongwa na ndege hiyo.